Ijumaa, 14 Julai 2017

Elizabeth Michael (Lulu) atwajwa kuwa ndiye mwanamke mzuri muigizaji Tanzania

Mtandao wa Africa Ranking umemtaja Lulu ndiye muigizaji wa kike mwenye mvuto zaidi nchini Tanzania. Mtandao huo umetoa taarifa kuhusu wanawake 10 waigizaji wenye mvuto zaidi nchini Tanzania.
Lulu akiwa na nguo yenye mvuto
Mtandao huo umetoa orodha ya waigizaji hao kama ifuatavyo:-

10. Mariam Ismail

Huyu muigizaji chipukizi ameonekana kujulikana Africa nzima na kuchukua nafasi ya 10. Muigizaji huyu ni miongozi mwa waigizaji katika SwahiliWood. Miongoni mwa kazi alizoshiriki ni pamoja na Omega Confusion, The return of Omega na zingine nyingi.
Mariam Ismail

9. Jennifer Kyaka (Odama)

Odama naye ametajwa kuwa ni moja ya waigizaji wenyemvuto Tanzania. Odama ambaye ni mwandishi wa filamu na vilevile producer, mtandao huo umemuweka kwenye nafasi ya 9 kati ya waigizaji wa kike 10. Kati ya filamu alizoshiriki ni pamoja na Pain Killer, Zebra, Witchdoctor na zingine nyingi.
Jennifer Kyaka (Odama)

8. Ivon Cheryl (Monalisa)

Ivon Cheryl anayejulikana kwa jina la Monalisa naye ni miongoni mwa waigizaji wa kitanzania wenye mvuto. Monalisa amewahi kushinda tuzo nyingi nchini Tanzania.
Ivon Cheryl (Monalisa)

7. Irene Uwoya

Irene Uwoya naye katajwa kuwa ni miongoni mwa wigizaji wenye mvuto Tanzania. Uwoya amewahi kuigiza filamu nyingi na kuvuta hisia za watu. Filamu zake zilileta mabadiliko makubw katika mtazamo mwa waigizaji wengi nchi Tanzania.
Irene Uwoya


6. Shilole

Zena Muhammed (Shilole), naye ametajwa kuwa ni miongoni mwa waigizaji wa kitanzani wenye mvuto. Shilole amewahi kuigiza filamu mbali mbali za kitanzania. Ni miongoni mwa waigizaji wa kike waliotajwa na mtandao huo.
Shilole

5. Aunt Ezekiel

Aunt Ezekiel alizaliwa jijini Dar es salaam, ni mtoto wa mchezaji wa mpira wa miguu Ezekiel Greyson. Ni moja ya waigizaji wa kike waliotajwa na mtandao huo kuwa ndio wenye mvuto zaidi Tanzania. 
Aunt Ezekiel

4. Jacqueline Wolper

Jacqueline Wolper naye ametajwa kuwa ni miongoni mwa waigizaji wa kike wenyemvuto nchini Tanzania. Aliingia kwenye kuigiza filamu mwaka 2007 na kuleta changamoto kubwa kwa waigizaji aliowakuta. Amewahi kushiriki katika filamu zaidi ya 20. Ametajwa kushika nafasi ya nne.
Jacqueline Wolper

3. Richa Adhia

Richa Adhia naye ametajwa kuwa ni miongoni wa waigizaji wa filamu za kitanzania wenye mvuto. Mrembo huyu amewahi kushinda mashindano ya Miss Earth Tanzania (2006), Miss Tanzania World (2007) and Miss India Tanzania (2010). Ametajwa kuchukua nafasi ya tatu.

Richa Adhia


2. Wema Sepetu

Wema Sepetu naye ametajwa kuwa ni miongoni mwa waigizaji wenye mvuto Tanzania. Wema ametajwa kuchukua nafasi ya pili.
Wema Sepetu

Kwa maelezo zaidi soma hapa





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni