Jiji la dar es salaam |
Hii ni kutokana na juhundi mbalimbali za wananchi wakishirikiana na serikali, ndio maana sasa nasi tumeanza kuonekana kimataifa. Hatutakiwi kubweteka sasa ni muda wa kujitahidi zaidi ili hapo baadae tuwe ni miongoni mwa majiji masafi duniani.
Zile tabia za kutpa tupa taka ovyo, tuache. Huku viongozi wa serikali za mitaa wakishiriki kikamilifu katika kuhamasisha usafi. Unajua tunapokuwa tunafanya usafi vizuri na jiji letu la Dar es salaam likawa safi, tutaweza kuvutia wawekezaji, watalii na isitoshe tutakuwa na afya njema.
Mtandao wa African Zeal umetaja na kueleza kuwa kati ya majiji 10 barani Afrika Dar es salaam imechukua nambari tisa. Ni kama hapo chini:
City | Country |
---|---|
1. Cape Town | South Africa |
2. Port Louis | Mauritius |
3. Johannesburg | South Africa |
4. Nairobi | Kenya |
5. Gaborone | Botswana |
6. Tunis | Tunisia |
7. Accra | Ghana |
8. Libreville | Gabon |
9. Dar es Salaam | Tanzania |
10. Windhoek | Namibia |
Unaweza ukasoma zaidi hapa ili upate maelezo zaidi:
http://www.africanzeal.com/cleanest-cities-in-africa/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni