Ijumaa, 14 Julai 2017

Elizabeth Michael (Lulu) atwajwa kuwa ndiye mwanamke mzuri muigizaji Tanzania

Mtandao wa Africa Ranking umemtaja Lulu ndiye muigizaji wa kike mwenye mvuto zaidi nchini Tanzania. Mtandao huo umetoa taarifa kuhusu wanawake 10 waigizaji wenye mvuto zaidi nchini Tanzania.
Lulu akiwa na nguo yenye mvuto
Mtandao huo umetoa orodha ya waigizaji hao kama ifuatavyo:-

10. Mariam Ismail

Huyu muigizaji chipukizi ameonekana kujulikana Africa nzima na kuchukua nafasi ya 10. Muigizaji huyu ni miongozi mwa waigizaji katika SwahiliWood. Miongoni mwa kazi alizoshiriki ni pamoja na Omega Confusion, The return of Omega na zingine nyingi.
Mariam Ismail

9. Jennifer Kyaka (Odama)

Odama naye ametajwa kuwa ni moja ya waigizaji wenyemvuto Tanzania. Odama ambaye ni mwandishi wa filamu na vilevile producer, mtandao huo umemuweka kwenye nafasi ya 9 kati ya waigizaji wa kike 10. Kati ya filamu alizoshiriki ni pamoja na Pain Killer, Zebra, Witchdoctor na zingine nyingi.
Jennifer Kyaka (Odama)

8. Ivon Cheryl (Monalisa)

Ivon Cheryl anayejulikana kwa jina la Monalisa naye ni miongoni mwa waigizaji wa kitanzania wenye mvuto. Monalisa amewahi kushinda tuzo nyingi nchini Tanzania.
Ivon Cheryl (Monalisa)

7. Irene Uwoya

Irene Uwoya naye katajwa kuwa ni miongoni mwa wigizaji wenye mvuto Tanzania. Uwoya amewahi kuigiza filamu nyingi na kuvuta hisia za watu. Filamu zake zilileta mabadiliko makubw katika mtazamo mwa waigizaji wengi nchi Tanzania.
Irene Uwoya


6. Shilole

Zena Muhammed (Shilole), naye ametajwa kuwa ni miongoni mwa waigizaji wa kitanzani wenye mvuto. Shilole amewahi kuigiza filamu mbali mbali za kitanzania. Ni miongoni mwa waigizaji wa kike waliotajwa na mtandao huo.
Shilole

5. Aunt Ezekiel

Aunt Ezekiel alizaliwa jijini Dar es salaam, ni mtoto wa mchezaji wa mpira wa miguu Ezekiel Greyson. Ni moja ya waigizaji wa kike waliotajwa na mtandao huo kuwa ndio wenye mvuto zaidi Tanzania. 
Aunt Ezekiel

4. Jacqueline Wolper

Jacqueline Wolper naye ametajwa kuwa ni miongoni mwa waigizaji wa kike wenyemvuto nchini Tanzania. Aliingia kwenye kuigiza filamu mwaka 2007 na kuleta changamoto kubwa kwa waigizaji aliowakuta. Amewahi kushiriki katika filamu zaidi ya 20. Ametajwa kushika nafasi ya nne.
Jacqueline Wolper

3. Richa Adhia

Richa Adhia naye ametajwa kuwa ni miongoni wa waigizaji wa filamu za kitanzania wenye mvuto. Mrembo huyu amewahi kushinda mashindano ya Miss Earth Tanzania (2006), Miss Tanzania World (2007) and Miss India Tanzania (2010). Ametajwa kuchukua nafasi ya tatu.

Richa Adhia


2. Wema Sepetu

Wema Sepetu naye ametajwa kuwa ni miongoni mwa waigizaji wenye mvuto Tanzania. Wema ametajwa kuchukua nafasi ya pili.
Wema Sepetu

Kwa maelezo zaidi soma hapa





Alhamisi, 13 Julai 2017

Dar es salaam ni miongoni mwa majiji 10 masafi Afrika

Africa inaeldelea kukua kwa kasi, huku jiji la Dar es salaam likiwa ni moja mwa majiji  masafi barani Afrika. Japo kuwa miaka kidogo ya nyuma ilionekana kuwa jiji la Dar es salaam ni miongoni mwa majiji machafu duniani. Kwa sasa Dar es salaam imetajwa kuwa ni miongoni mwa majiji kumi masafi barani Afrika.
Jiji la dar es salaam


Hii ni kutokana na juhundi mbalimbali za wananchi wakishirikiana na serikali, ndio maana sasa nasi tumeanza kuonekana kimataifa. Hatutakiwi kubweteka sasa ni muda wa kujitahidi zaidi ili hapo baadae tuwe ni miongoni mwa majiji masafi duniani.

Zile tabia za kutpa tupa taka ovyo, tuache. Huku viongozi wa serikali za mitaa wakishiriki kikamilifu katika kuhamasisha usafi. Unajua tunapokuwa tunafanya usafi vizuri na jiji letu la Dar es salaam likawa safi, tutaweza kuvutia wawekezaji, watalii na isitoshe tutakuwa na afya njema.

Mtandao wa African Zeal umetaja na kueleza kuwa kati ya majiji 10 barani Afrika Dar es salaam imechukua nambari tisa. Ni kama hapo chini:

CityCountry
1. Cape TownSouth Africa
2. Port LouisMauritius
3. JohannesburgSouth Africa
4. NairobiKenya
5. GaboroneBotswana
6. TunisTunisia
7. AccraGhana
8. LibrevilleGabon
9. Dar es SalaamTanzania
10. WindhoekNamibia

Unaweza ukasoma zaidi hapa ili upate maelezo zaidi:
http://www.africanzeal.com/cleanest-cities-in-africa/

Prof. Mdoe afanya mazungumzo na uongozi wa Uranium One


Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Uranium One na Mantra Tanzania ambao wanamiliki leseni ya uchimbaji wa Madini ya Urani kwenye eneo la Mto Mkuju Kusini mwa Tanzania. Mantra ni sehemu  ya  kampuni ya Uranium One na kampuni ya kimataifa ya madini ya ROSATOM-ya Shirikisho la Serikali ya Urusi ya Nishati ya Nyuklia.

Kaimu Katibu Mkuu,Wizara ya Nishati na Madini,  Profesa James Mdoe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Uranium One, Vladimir Hlavinka katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam. Katikati ni Rais wa Uranium One Group, Vasility Konstantinov.


Kikao hicho kilijadili masuala mbalimbali ikiwemo ushirikiano kati ya Tanzania na kampuni hizo, kuporomoka kwa bei ya Urani katika soko la dunia na kampuni hizo kushirikiana na STAMICO katika miradi ya uzalishaji madini.

Rais wa Uranium One Group, Vasility Konstantinov aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano inaoendelea kuutoa kwa kampuni hizo ili kuhakikisha kuwa lengo la kampuni hiyo kuendeleza mradi wa uchimbaji madini ya urani nchini linafanyika kwa ufanisi.

Konstantinov pia alitumia nafasi hiyo kukanusha habari zilizoandikwa katika baadhi ya magazeti nchini hivi karibuni kuwa kampuni ya MANTRA Tanzania imesitisha (Suspension) uchimbaji wa Madini ya Urani kwenye leseni yao iliyoko eneo la Mto Mkuju moja ya sababu ikiwa ni mabadiliko katika Sheria ya Madini.

Soma maelezo mengine hapa:
https://issamichuzi.blogspot.com/2017/07/prof-mdoe-afanya-mazungumzo-na-uongozi.html

Mchezaji anayekusudiwa na Sunderland hakujumuisha kwenye timu ya Everton

Mchezaji wa mpira wa Everton Aiden McGeady hajaweza kuja pamoja na timu yake nchini Tanzania. Hii huenda ni kutokana na makusudio ya timu ya Sunderland kumchukua. Mezaji huyo mwenye asiri ya Ireland hajaonekana kuwepo kwenye timu ya Everton iliyowasili nchini Tanzania

 Aiden McGeady alizaliwa 4 April 1986 na kwa sasa akiwa na umri wa miaka 31. Huku akiwa na urefu wa futi 5 na inchi 11, huenda kajiunga na timu ya Sunderland.
Maelezo hayo yamelipotiwa na mtandao wa "http://www.sunderlandecho.com" yameonesha kwamba japo kuwa malipo bado lakini mchezaji hajaonekana kwenye safari hiyo.

 Aiden McGeady akiimba wimbo wa taifa wa nchi yake mwaka 2013


Soma zaidi hapa: http://www.sunderlandecho.com/sport/football/sunderland-afc/sunderland-target-not-included-in-everton-squad-for-tanzania-trip-1-8644584